Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu katibu Mkuu atoa mwito wa kusaidiwa mataifa ya Afrika magharibi yaliyokumbwa na vita

Naibu katibu Mkuu atoa mwito wa kusaidiwa mataifa ya Afrika magharibi yaliyokumbwa na vita

Naibu katibu mkuu Asha-Rose Migiro ametowa mwito wa kuungwa mkono zaidi Guinea-Bissau na mataifa mengine katika kanda hiyo, ambayo yana jikokota kutoka hali ya vita. Alisema hayo baada ya kurudi New York, kufuatia ziara yake ya Afrika wiki iliyopita.