Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

. Walinda amani wa Jordan katika kikosi cha UM huko Ivory Coast wametoa madawa kwa taasisi ya elimu huko mjini Cocody kama sehemu ya juhudi zao za huduma za dhaura kusaidia taifa hilo lililogawika mapande mawili. Kamanda wa kikosi chao Kanali Ali Bairat alisema msaada huo una lengo la kusaidia kupambana na malaria na ni sehemu ya shughuli za huduma za dharura zinazofanywa na wajumbe wa amani kutoka Jordan, ili kusadia kupunguza maafa kwa raia wa kawaida. ~

. Baraza la usalama limeongeza hadi Januari 2008 muda wa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa huko Ivory Coast na vikosi vya Ufaransa vinavyo isaidia kutayarisha uchaguzi huru na wa haki katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi. Kwa sauti mmoja, baraza liliidhinisha azimio linalofutilia mbali madaraka ya mjumbe maalum wa UM kwa ajili ya uchaguzi huko Ivory Coast, Bw Gerard Stoudmann, na kumkabidhi mjumbe huyo maalum wa Ban Ki-moon nchini humo, jukumu la kuidhinisha kila awamu ya utaratibu wa uchaguzi.

. Katibu mkuu Ban Ki-moon ametoa mwito wa kuwepo na ulinzi mkubwa zaidi kwa ajili ya watoto wanao jikuta katika migogoro katika mataifa ya Chad na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Bw Ban alitoa onyo lake katika ripoti mbili kuhusiana na ukiukaji mkubwa wa haki za watoto na za binadamu huko Chad pamoja na kuwandikishwa watoto katika jeshi la taifa la Chad, makundi ya upinzani ya wapiganaji, na waasi wa Sudan wanaoendesha shughuli zao kaika nchi jirani.