Skip to main content

UNESCO yatangaza washindi wa tunzo ya 2007 ya kupambana na kutokujua kuandika

UNESCO yatangaza washindi wa tunzo ya 2007 ya kupambana na kutokujua kuandika

Shirika la UM la Elimu na Sayansi la UM, UNESCO liliwatangaza washindi watano wa tunzo yake ya kupambana na kutojua kuandika na kusoma mwaka huu. Washindi hao watano kutoka China, Marekani, Nigeria, Senegal na Tanzania wametambuliwa kwa juhudi zao za kuwaelimisha watu kusoma na kuandika, kipau mbele moja wapo cha UNESCO.