Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la uhamiaji

Tatizo la uhamiaji

TY:Tukiendelea na makala ya Jarida wiki hii, tunazungumzia tatizo la uhamiaji, ambalo limekua likijadiliwa sana mwezi huu hasa wakati wa mkutano wa kimataifa juu ya uhamiaji na maendeleo mjini Brussels, Ubelgiji.

AA: Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia kikao cha ufunguzi wa mkutano wa kimataifa, alitoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka na thabiti kutanzua matatizo makubwa yanayo wakabili wahamiaji milioni 200 duniani. Alisema tatizo hilo ni moja wapo ya changa moto kuu za karne hii.

CutBan International migration is an issue ..

AA:Uhamiaji wa kimataifa ni suala muhimu kabisa katika karne ya 21. vile vile ni suala gumu na lenye utata mkubwa kufahamu kwa ukamilifukuna mengi yaliyo hatarini kuanzia haki wahamiaji, mabilioni ya fedha kwa ajili ya uwekezaji muhimu kabisa katika maendeleo na ukuwaji wa uchumi inabidi tufanye kazi kwa pamoja alisema.

AAKwa upande wa Afrika, hali imezidi kua mbaya zaidi kukiwepo na mamia na mamia ya watu wakitumia boti zisizo na usalama kusafiri kutoka Senegal hadi visiwa vya Canary vinavyo tawaliwa na Hispania, au kuvuka ghuba ya Aden kutoka Somalia hadi Yemen, pamoja na wengine wanaovuka bahari ya Mediterranean kutoka Afrika ya Kaskazini hadi Ulaya. Watu hao wote wanatoa fidia maisha yao ili kwenda kutafuta maisha bora huko Ulaya. Msemaji wa shirika la wakimbizi la UM, UNHCR, Bi Jennifer Pagonis, anasema idadi ya wanaovuka kuingia Yemen imepunguka mwaka huu lakini watu wengi zaidi wanafariki baharini.

Cut Pagonis.. for the first six months of the year we recorded the arrival of

AKKwa miezi sita ya kwanza ya mwaka huu tume orodhesha kuwasili kwa maboti 77 ya biashara ya magendo ikiwasafirisha wakimbizi, wahmiaji na wanaotafuta hifadhi elfu nane mia sita hasa kutoka Somalia na Ethopia. Na katika kipindi hicho hicho, watu 367 walifariki na karibu 118 hawajulikani wako wapi. Na katika kipindi hicho hicho mwaka jana, ni watu mia mbili na sitini walofariki na watu elfu kumi na moja mia saba walovuka ghuba.

AABi Pagonis anasema, wahamiaji wana rubuniwa na wafanyabiashara magendo makatili wasio jali maisha ya binadamu kwa kuwalipisha fedha chungu nzima kuwavukisha na hatimae kuwatupa baharini kabla ya kuwasili pwani ya Yemen. Anasema Kuna ukatili wa aina mbali mbali unaofanyika. Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, Jemini Pandya anasema shirika lake linawasaidia waafrika wengine pia wanaojaribu kufika nchi za Ulaya kwa maboti ya hatari.