Kwa habari za hapa na pale

27 Julai 2007

Mashirika ya huduma za dharura ya UM yanapeleka kwa haraka misaada ya chakula na afya kusini mwa Sudan ambako mvua kali mnamo siku za hivi karibuni zimesababisha mafuriko yaliyowathiri karibu watu elfu 10. Shirika la watoto la UM, UNICEF limeshapeleka mikoba midogo 1 500 madawa na vitu vya dharura, pamoja na chakula cha siku 15.

Program ya Chakula Duniani WFP imeonya wiki hii kwamba makumi elfu ya watoto huko Benin hawatopata chakula cha kila siku shuleni wakati shule zitakapofunguliwa Septemba hadi pale fedha zaidi zinapatikana. Mpango wa kuwalisha wanafunzi shule unaosimamiwa na WFP una wasiadia karibu watoto elfu 70 katika shule 400, unahitaji dola milioni moja haraka. Utafiti umeonesha kwamba kupata angalau chakula mara moja kwa siku shuleni, haiepushi njaa pekee bali ina imarisha uwezo wa kusoma kwa mwanafunzi. Kutolewa chakula pia ni moja wapo ya mambo inayowapatia familia motisha kuwapeleka watoto wao shule hasa wasichana.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter