Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano juu ya mzozo wa Darfur unmepangwa kufanyika mapema Augusti.

Mkutano juu ya mzozo wa Darfur unmepangwa kufanyika mapema Augusti.

Wajumbe maalum wa UM na AU wakiendelea na juhudi za kutafuta suluhisho la kisiasa kwa ajili ya ugomvi wa jimbo la Darfur huko Sudan, wamewaalika viongozi wa makundi ambayo hayakutia sahihi makubaliano ya amani kwa mazungumzo ya ‘majadiliano ya awali’ yaliyopangwa kuanza mapema mwezi ujao huko Arusha Tanzania.

Katika taarifa iliyotolewa mjini Khartoum wiki hii, wajumbe maalum Salim Ahmed Salim wa Au na Jan Eliasson wa UM wanasema washirika walotoa msaada kwa ajili ya utaratibu wa kisiasa wataalikwa pia kuhudhuria mkutano huo wa tarehe 3 Augusti pamoja na viongozi wa makundi ambayo hayakutia sahihi makubaliano ya amani ya Darfur. Lengo la mazungumzo ya Arusha kutathmini yaliyokwisha patikana hadi hivi sasa na kuzingatia juu ya jukumu kuu la kila upande wa vyama vya Sudan kuhakikisha majadiliano ya haraka na kupatikana suluhisho la kudumu kwa mzozo wa Darfur na kuamua mahala na watakao shiriki katika majadiliano.