Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa kwanza wa Zambia kwa WFP unasaidia kupunguza upungufu wa chakula.

Msaada wa kwanza wa Zambia kwa WFP unasaidia kupunguza upungufu wa chakula.

Program ya Chakula Duniani WFP, imepongeza mchango wa kwanza kabisa kutoka kwa serekali ya Zambia, ambao utawawezesha maelfu ya wa Zambia kupokea msaada muhimu wa chakula baada ya Septemba.

Mwakilishi wa WFP nchini Zambia David Stevenson amesema, mchango huo umefika kwa muda muafaka kabisa na utaepusha hatua zozote za haraka za kupunguza mipango yake ya dharura huko Zambia. Kwa mara ya kwanza kabisa serekali ya Lusaka imetoa mchango wa tani elfu 10 za mahindi yenye thamani ya dola milioni mbili na nusu. Bw Stevenson ameishukuru serekali ya Lusaka na kusema mchango utaokowa maisha ya watu wadhaifu kote nchini, pamoja na maelfu ya wagonjwa wa ukimwi, mayatima na familia zao.