Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yatoa mwito kwa pande zote Sierra Leone kuepusha ghasia kabla uchaguzi.

UM yatoa mwito kwa pande zote Sierra Leone kuepusha ghasia kabla uchaguzi.

UM umetoa mwito kwa vyama vyote vya kisiasa huko Sierra Leone kujiepusha kutumia matusi na maneno ya uchochezi yanayoweza kusababisha ghasia kabla ya uchaguzi wa rais na wa bunge wa mwezi ujao. Mwakilishi maalum wa katibu mkuu Victor Angelo akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa mkutano wa kitaifa juu ya majadiliano na vijana alisema, inabidi tufahamu matukiyo ya hivi karibuni ya ghasia za kisiaasa.

Alisema ana viomba vyama vya kisiasa kujitenga kabisa na aina yeyote ya ghasia za kisiasa, akisema viongozi wa kisiasa wana jukumu maalum na lazima watowe muongozo kwa wafuasi wao. Huu ni uchaguzi wa pili wa kidemokrasia tangu Sierra Leone kumaliza vita virefu vya wenyewe kwa wenyewe. Na Wiki hii afisi ya UM huko Sierra Leone na tume ya taifa ya uchaguzi wamemaliza kutowa mafunzo kwa karibu maafisa 50 wa wilaya kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.