Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa Darfur unavyosababisha matatizo ya usalama kwa majirani wa Sudan.

Mzozo wa Darfur unavyosababisha matatizo ya usalama kwa majirani wa Sudan.

Wakati majadiliano yanaendelea kwenye baraza la usalama katika kumaliza kuandika azimio litakalo ruhusu kupelekwa kwa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Jumuia ya afrika huko Darfur, mzozo huo katika eneo la magharibi ya Sudan umekua na athari kubwa kwa majirani zake Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Tatizo la pili ambalo ni la hivi karibuni linalotokana hasa na kupanuka kwa mzozo wa Darfur hadi nchi za jirani ni zozo la watu walokimbia makazi yao na wamebaki Chad. Hii leo kuna watu elfu 170, na inabidi kusisitiza kwamba idadi yao iliongezeka saana mwishoni mwamwaka 2006.

Hali ya huko mashariki ya Chad ni ya kutatanisha kabisa, kutokana na ukweli kwamba wakati eneo hilo limewapokea wakimbizi kutoka Drafur, kuna pia wa Chad walokwenda kuka Darfur katika ardhi zilizoachwa wazi na watu walokimbia kutoka Darfur. Na hali hiyo imesababisha kuenea kwa uvumi kwamba wakuu wa Sudan wanataka kuwapeleka wakimbizi wa kutoka Chad kuishi katika maeneo hayo. Mwakilishi wa UNHCR huko Sudan Chris Ache hamini kuna ukweli katika tuhuma hizo, kwani yeyote anadai kua ni mkimbizi lazima awekwe katika kambi ya wakimbizi.

Ninachoweza kusema ni kwamba hatuna ushahidi kwamba kuna mpango mkubwa wa serekali kuwahamisha wakazi kuishi Darfur ya Magharibi. UNHCR na washirika wetu mnamo miezi miwili iliyopita tumeshapeleka karibu tume 24 za uchunguzi katika maeneo tofauti wanaoishi wakimbizi. Tumezungumza nao na kumefikia uwamuzi kwamba kweli wanatokea Chad.

Licha ya takwimu hizo na utata mkubwa katika mzozo kamili Serge Male anawakumbusha wanadishi habari kwamba, watu hao wameona maafa makubwa, hata hivyo kuna matumaini. Jumuia ya Ulaya imetanagaza wiki hii inafikiria kupeleka jeshi la amani kwenye eneo la mipaka ya nchi hizo tatu. Wanajeshi hao wakipelekwa basi kutasaidia sana kubadilisha hali ya maisha ya watu ndani ya makambi mashariki ya Chad na bila shaka hali nzuri ya kufanya kazi za huduma za dharura.