Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukumbu juu ya kikao cha 2007 cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili

Kumbukumbu juu ya kikao cha 2007 cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili

Makala yetu wiki hii itazingatia maoni ya Catherine Mututua, anayewakilisha shirika lisio la kiserekali la Kenya linaloitwa NAMAYANA kuhusu kikao cha sita cha Tume ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili Duniani, ambaye anaelezea matarajio aliokuwa nayo juu ya uwezekano wa kuwatekelezea wenyeji hao haki zao kamili katika siku zijazo.

Kikao cha 2007 cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili, kilichofanyika Makao Makuu ya UM mjini New York, kilipata fursa ya kusikiliza taarifa na ripoti nyingi kutoka kwa wajumbe wa kimataifa mbalimbali waliowakilisha kanda kadha wa kadha za dunia ambazo zilielezea matatizo yanayowakabili fungu hili la umma wa kimataifa kila siku katika juhudi zao za kuendeleza maisha ya kawaida. Asilimia kubwa ya wajumbe waliohutubia vikao vya Tume walilalamika ya kuwa, mara nyingi wenye madaraka huwapuuza na kuwatenga wakati wanapozingatia zile sera zinazoambatana na umiliki wa ardhi, utawala wa maeneo ya kijadi na fursa ya kuekeza vitega uchumi kwa kutumia mali ya asili, utajiri ambao mara nyingi hutikana kwenye maeneo ya jadi ya wenyeji wa asili.

Sikiliza mahojiano kamili na C. Mututua kwenye idhaa ya mtandao.