Hapa na pale
KM Ban Ki-moon amepokea kwa moyo thabiti maafikiano yaliofikiwa na viongozi wa kundi la G-8 kwenye mji wa Heiligendamm, Ujerumani ambapo walikubaliana kuchukua hatua za mapema, na zenye nguvu kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani, na kuahidi kutumia mfumo wa Umoja wa Mataifa (UM) katika kuitekeleza miradi hiyo.
Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti kuwa gharama za kuagizishia chakula duniani karibuni zimeongezeka kwa kima kikubwa sana kwa sababu ya kupanda kwa bei ya nishati ya viumbe hai, kitendo ambacho kilikiuka rikodi ya mwaka jana.
Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO) limeripoti ya kwamba utafiti wao umethibitisha mfanyakazi mmoja katika kila wafanyakazi watano duniani hukiuka masaa ya kawaida kwenye vibarua wanavyovitumikia kuweza kuazalisha pato la kuridhisha kuendesha maisha na kukidhia mahitaji ya aila zao.