Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya chakula katika Zimbabwe inaregarega; UNICEF kusaidia kuchanja watoto dhidi ya polio

Hali ya chakula katika Zimbabwe inaregarega; UNICEF kusaidia kuchanja watoto dhidi ya polio

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) pamoja na mashirika wenzi yameanzisha kampeni ya pamoja ya kuwapatia watoto milioni 2 nchini chanjo dhidi ya maradhi ya kupooza (polio) katika Zimbabwe, hasa ilivyokuwa asilimia kubwa ya raia inakabiliwa na matatizo yanayosababishwa na kuporomoka kwa maendeleo ya uchumi kitaifa.

Kadhalika, Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) yametangaza ripoi bia iliothibitisha kwamba thuluthi moja ya jumla ya watu milioni 12 nchini Zimbabwe watakabiliwa na tatizo la upungufu mkubwa wa chakula baina ya kipindi tuilokuwemo sasa hivi hadi mwanzo wa mwaka ujao, kwa sababu mwaka huu mavuno ni haba na mzozo wa uchumi bado unaendelea kukithiri nchini.