Usomali kufadhiliwa msaada wa kihali na UM
Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Misaada ya Dharura ya Kiutu (CERF) inatarajiwa kuifadhilia Usomali msaada wa dola miloni 3 ambazo zitatumiwa kupeleka kwenye yale maeneo ya Mogadishu yalioathirika na mapigano, kwa kutumia usafiri wa ndege, wafanyakazi wa mashirika yasio ya kiserekali na kupeleka misaada ya kihali kwa umma muhitaji. Kwa mujibu wa taarifa za UM eneo la Usomali sasa linakabiliwa na tatizo la mvua, hali ambayo huzorotisha huduma za usafiri wa kwenye barabara.