Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika kutawala ajenda ya Baraza la Usalama mwezi Juni

Afrika kutawala ajenda ya Baraza la Usalama mwezi Juni

Balozi Johan C. Verbeke wa Ubelgiji, ambaye taifa lake limeshika madaraka ya uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Juni, aliwaambia waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu kuwa kwamba anaashiria kuwepo “ajenda nzito” katika mijadala ya mwezi huu ya Baraza, na wingi wa mada zitakazozingatiwa kwenye Baraza, alisisitiza, zitahusu masuala ya Afrika.

Kadhalika, Balozi Verbeke alisema ya kuwa kuanzia wiki ijayo wajumbe wa Baraza la Usalama wanatazamiwa kufanya ziara ya wiki moja barani Afrika, na wanatazamiwa kuzuru Ghana, Ethiopia, Sudan, Cote d’Ivoire na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.