Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya mhudumia misaada ya kiutu katika CAR

UM walaani mauaji ya mhudumia misaada ya kiutu katika CAR

John Holmes, Makamu KM juu ya Masuala ya Kiutu na Mshauri wa Misaada ya Dharura amelaani vikali mauaji ya Elsa Serfass mfanyakazi wa shirika linalotoa huduma bure za afya la Medecins sans Frontiere, mauaji ambayo yalitukia katika eneo la kaskazini-magharibi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Holmes alisema ana wasiwasi na kuharibika kwa hali ya usalama hivi karibuni katika eneo la kaskazini-magharibi ya nchi. Alitoa mwito kwa makundi yote husika na mgogoro wao kuhakikisha wafanyakazi wa huduma za kiutu wanapatiwa hifadhi ifaayo na kuwapatia usalama kwa umma muhitaji.