Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan yakubali vikosi vya mseto vya kimataifa kwa Darfur

Sudan yakubali vikosi vya mseto vya kimataifa kwa Darfur

Baada ya kufanyika mashauriano ya kiufundi, ya siku mbili, kwenye mji wa Addis Ababa, Ethiopia katika wiki hii, kati ya wawakilishi wa UM na wale wa kutoka AU, pamoja na wajumbe wa Serekali ya Sudan, kulidhihirika fafanuzi za kuridhisha juu ya yale masuala yaliokuwa yakikwamisha utekelezaji wa mpango wa kupeleka vikosi vya mseto kulinda amani katika jimbo la magharibi la Darfur. Baada ya kikao cha Addis Ababa kulitolewa taarifa ya pamoja kati ya Serekali ya Sudan na AU iliosema ya kuwa Sudan imeridhia na kuidhinisha ule mpango wa kupeleka vikosi vya mseto vya UM na AU kwenye jimbo la Darfur.

Mtayarishaji vipindi AZR alipata fursa ya kuzungumza na Jumbe Omar Jumbe, Afisa wa Habari wa Shirika la UM juu ya Operesheni za Amani Sudan (UNMIS) ambaye alihudhuria kikao cha wanahabari kufuatia maafikiano hayo. Kwanza Bw Jumbe aliulizwa hasa ni mambo gani yalitakiwa yarekibishwe mbeleni kabla ya Sudan kuidhinisha mpango wa kupeleka majeshi ya amani ya mseto katika Darfur?

Sikiliza dokezo ya mahojiano kwenye idhaa ya mtandao.