Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

William Clay, Mtaalamu wa UM juu ya lishe bora wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) ameripoti kwamba kumethibitishwa mabibi au nyanya, ni fungu la umma wa kimataifa muhimu linalojumuisha rasilmali kubwa ya kutumiwa mara kwa mara katika huduma za maendeleo, hasa katika ulezi na udhibiti wa lishe bora kwa watoto, na katika utunzaji wa afya ya jamii.~

Ripoti ya karibuni ya Baraza la Kusimamia Maendeleo ya Uchumi kwa Afrika (ECA) imedokeza ya kuwa ubaguzi wa kijinisa dhidi ya wanawake barani Afrika unawanyima wanawake mafanikio kwenye harakati za ujasirimali na kuendesha biashara; na ilipendekezwa kufanyike marekibisho kwenye miradi ya maendeleo na sera za taifa kuhakikisha wanawake wanahusishwa kikamilifu kwenye huduma hizi za kiuchumi bila pingamizi.

Wajumbe wanaowakilisha mataifa 13 ya Bahari ya Hindi walikutana Mauritius wiki hii, chini ya uongozi wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), kujadilia taratibu za kuimarisha usalama wa bandari zao dhidi ya biashara ya uvuvi haramu, hususan katika zile sehemu za magharibi na pia katika mwambao wa mashariki ya Afrika.

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu lilikamilisha kikao chake cha tano tarehe 19 Juni baada ya kupitisha karibu saa sita za usiku furushi la maazimio yaliopendekezwa na Raisi wa Baraza hilo, maazimio ambayo yalijumuisha maafikiano juu ya mfumo mpya wa kufanyisha Mapitio ya Mara kwa Mara kwa Kila Nchi Mwanachama kuhusu namna haki za binadamu zinavyotekelezwa katika maeneo yao.

David Shearer, mkuu wa Ofisi ya Misaada ya Dharura ya Kiutu (OCHA) kwenye maeneo yaliokaliwa kimabavu ya Wafalastina aliwaambia wanahabari katika Makao Makuu Alkhamisi kwamba hali ya kimaisha ndani ya Tarafa ya Ghaza itaendelea kuharibika pindi Israel itakakamaa kutoondosha vikwazo au kutofungua vituo vya kuvukia mipaka kwenye maeneo yaliofunikwa na mapigano.

[na hatimaye] Larry Johnson, KM Mdogo anayehusika na Masuala ya Sheria ametoa mwito unaohadharisha kuchukuliwa uangalifu mkubwa na ushirikiano kati ya Mataifa Wanachama dhidi ya ugaidi, na ameyataka mataifa wanachama kuidhinisha haraka mkataba mpya wa kujikinga na matishio ya alichokiita ugaidi wa kinyuklia.