Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inaiomba Kenya kuruhusu misaada ya chakula Usomali

WFP inaiomba Kenya kuruhusu misaada ya chakula Usomali

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (WFP) limetoa mwito maalumu unaoisihi Serekali ya Kenya kuruhusu malori 140 yaliokodiwa na UM na yaliochukua shehena za chakula, kuvuka mpaka wa kaskazini-mashariki na kuingia Usomali.

Operesheni za WFP ZA kupeleka misaada ya chakula Usomali kusini zilisimamishwa ghafla mipakani na Serekali ya Kenya kuanzia tarehe 25 Mei mwaka huu. Jumla ya malori yalioselelea mipakani kwa sasa ni 290 yenye shehena ya tani za metriki 8,500 za chakula na vifaa vyengine vya misaada ya kihali.