Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNEP yahusisha mabadiliko ya hali ya hewa na mifumko ya vurugu Sudan

Ripoti ya UNEP yahusisha mabadiliko ya hali ya hewa na mifumko ya vurugu Sudan

Fafanuzi za utafiti wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) zimethibitisha ya kwamba hakuna dalili Sudan itafanikiwa kudumisha usalama na amani katika nchi bila ya kudhibiti kidharura uharibifu wa kasi wa mazingira.

Kwa sababu ya kupungua kwa mvua, mavuno nayo pia yanaashiriwa kuporomoka kwa asilimia 70 hasa katika yale maeneo dhaifu yaliobanwa kimazingira.