Tume ya Baraza la Usalama imemaliza ziara ya wiki moja Afrika

Tume ya Baraza la Usalama imemaliza ziara ya wiki moja Afrika

Wajumbe 15 wanachama wa Tume ya Baraza la Usalama waliozuru mataifa matano ya Afrika kwa wiki moja walikamilisha ziara yao Ijumatano, tarehe 20 Juni katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) anbapo walifanya mazungumzo na watumishi wa UM waliopo huko pamoja na kuonana kwa mashauriano na Raisi Joseph Kabila na maofisa kadha wa Serekali.

Tume ya Baraza la Usalama ilianza ziara yake ya Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia na baadaye kuelekea Sudan, Ghana na Cote d’Ivoire kwa makusudio ya kushauriana na mataifa husika juu ya taratibu za kuchukuliwa kipamoja kuhakikisha usalama na amani zinadumishwa katika maeneo yao. Wajumbe wa Baraza la Usalama walirejea New York Alkhamisi, tarehe 22 Juni.