Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kuwakumbuka Wahamiaji Duniani

Siku ya Kuwakumbuka Wahamiaji Duniani

Ijumatano ya tarehe 20 Juni mwaka huu iliadhimishwa katika sehemu kadha wa kadha za ulimwengu kuwa ni ‘Siku ya Wahamiaji Duniani’, kumbukumbu zilizoshika fora katika kipindi ambapo pia kulitolewa mwito muhimu unaohimiza jumuiya ya kimataifa kukuza ushirikiano wao katika kuwasaidia wenziwao waliofurushwa makwao na kunyimwa makazi na maskani. Kadhalika mnamo siku hiyo kuliwasilishwa onyo lenye kuhadharisha walimwengu ya kwamba idadi ya wahamaji huenda kuongezeka katika kipindi kijacho.

Risala ya kuadhimisha ‘Siku ya Wahamiaji Duniani’ iliotolewa na KM Ban Ki-moon kwa mara ya kwanza tangu kushika madaraka ya kuwa mkuu wa taasisi ya UM, ilisisitiza kwamba kunahitajika kuwepo ushikamano wa kimataifa katika kuyakamilisha inavyostahiki majukumu ya kiutu ya dharura kwa wahamiaji muhitaji pamoja na kwa ule umma uliolazimishwa kuhajiri makazi kidharura. Ushikamano huu ni muhimu sana, alitilia mkazo KM.

Sikiliza taarifa kamili.