Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wenyeji wa asili watunza utamaduni wa kijadi kwa kutumia mawasiliano ya kisasa

Wenyeji wa asili watunza utamaduni wa kijadi kwa kutumia mawasiliano ya kisasa

Viongozi wa wenyeji wa asili walioshiriki kwenye mijadala ya kikao cha karibuni cha mwaka, cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Masuala ya Haki za Wenyeji wa Asili walisisitiza kwenye risala zao, kwa kauli moja, ya kwamba haiyafalii Mataifa Wanachama kuendelea kupoteza wakati katika kipindi cha kihistoria ambapo kunahitajika kuuidhinisha halan ule mwito wa Baraza la Haki za Binadamu wa kukomesha ubaguzi dhidi ya wenyeji wa asili, na kuupatia umma huu uliotengwa kijamii haki zao halali, hasa kwenye juhudi za kudhibiti na kutunza ardhi na rasilmali ziliopo kwenye maeneo yao.

Mohamed Yunus Rafiq alihudhuria kikao cha mwaka 2007 cha Tume ya Haki za Wenyeji wa Kiasili kwa niaba ya chama kisicho cha serekali cha Wamaasai wa Tanzania chenye mradi wa kutunza utamaduni kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kisasa.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.