Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kimataifa kupiga vita utekaji nyara wa watoto Afrika

Juhudi za kimataifa kupiga vita utekaji nyara wa watoto Afrika

Majuzi wawakilishi wa mataifa zaidi ya 10 kutoka Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu walikusanyika mjini Kampala, Uganda kwenye mkutano wa Shirika la UM dhidi ya Jinai na Madawa ya Kulevya (UNODC), na walizingatia ratiba ya sheria imara dhidi ya biashara ya magendo ya kuteka nyara watu na watoto, na kuwavusha mipaka kutoka makwao na kuwapeleka kwenye maeneo mengineyo kuendeleza ajira haramu, ya lazima, inayotengua kabisa haki za kibinadamu.~~

Mfanyakazi wa Ofisi ya Habari ya UM Nairobi, Irene Mwekesi alimhoji Profesa Philista Onyango ambaye alishiriki kwenye mkutano huo.

Sikiliza mukhtasari wa mahojiano.