Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeanzisha mradi mpya utakaotumiwa kuwakinga wagonjwa dhidi ya hatari ya makosa wakati wanapopimwa afya, hasa ilivyokuwa mgonjwa mmoja katika kila wagonjwa 10 kwenye nchi zinazoendelea hudhurika kiafya, kwa sababu ya utambuzi wa maradhi usio sahihi.~

• KM Ban Ki-moon alikuwa mmoja wa wenyekiti wawili walioongoza Mkutano wa Maafikiano ya Kimataifa Kuisaidia Iraq uliofanyika Sharm el-Sheikh, Misri kwa lengo la kufufua, nchini, huduma za kiuchumi, utulivu wa shughuli za kisiasa na vile vile kudumisha hali ya usalama mnamo miaka mitano ijayo.

• Robert Benson wa Kanada ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ofisi ya UM juu ya Masuala ya Maadili, Haki na Usawa kwa watumishi wa UM.