Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo vya almasi Liberia kuondoshwa na Baraza la Usalama

Vikwazo vya almasi Liberia kuondoshwa na Baraza la Usalama

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Liberia, Alan Doss amepongeza uamuzi wa karibuni wa Baraza la Usalama, wa kuondoa vikwazo dhidi ya biashara ya kuuza almasi kutoka taifa hili la Afrika Magharibi.

Vizuizi viliwekwa miaka sita nyuma ili kukomesha biashara ya almasi zilizojulikana, kwa umaarufu kama, ‘almasi za damu’, ambazo mapato yake yalitumiwa na Liberia, katika kipindi hicho, kuchochea uhasama na mapigano Afrika Magharibi.