Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

--FAO kupendekeza marekibisho ya ugawaji wa chakula katika nchi zinazoendelea--Utekelezaji wa haki za binadamu katika Darfur

--FAO kupendekeza marekibisho ya ugawaji wa chakula katika nchi zinazoendelea--Utekelezaji wa haki za binadamu katika Darfur

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) hivi karibuni liliwasilisha ripoti ya mwaka ambayo ilifanya mapitio juu ya Hali ya Chakula na Kilimo Duniani, ripoti ambayo hujulikana kwa umaarufu kama Ripoti ya SOFA. Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jacques Diouf alipoiwakilisha kwa mara ya kwanza ripoti hiyo alikumbusha ya kwamba wakati umewadia, kwa wahisani wa kimataifa kurekibisha huduma za ugawaji wa misaada ya chakula duniani.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Sehemu ya pili ya kipindi inazingatia shughuli za UM katika jimbo la Darfur, Sudan zinazoambatana na haki za binadamu.

Innocent Balemba Zahinda, ni mfanyakazi wa Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani kwa Sudan (UNMIS), ofisa anayesimamia kitengo kinachohusika na masuala ya haki za binadamu katika mji wa Nyala, Darfur ya Kusini. Mwandishi habari wa Redio ya UM, Israa Hamad alizuru eneo hilo karibuni na alipata fursa ya kumhoji Zahinda juu ya hali kwenye eneo, kwa ujumla.

Sikiliza mahojiano kwenye idhaa ya mtandao.