Mradi wa kudhibiti homa ya manjano kuanzishwa na WHO Afrika Magharibi
Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO), ambalo linakutana sasa hivi Geneva, Uswiss limepitisha mradi wa kuanzisha kampeni ya kudhibiti homa ya manjano katika mataifa 12 yaliopo Afrika Magharibi. Kwa mujibu wa WHO maradhi ya homa ya manjano yaligunduliwa kuibuka katika baadhi ya sehemu za Afrika Magharibi na kunahitajika juhudi za dharura kuyadhibiti yasije yakafumka kwa kasi na kulitapakaza janga hilo kwa umma uliobanwa na matatizo kadha mengineyo ya kiuchumi na jamii.