Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muda wa operesheni za UM katika DRC umeongezwa na Baraza la Usalama

Muda wa operesheni za UM katika DRC umeongezwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni za Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (DRC), yaani MONUC, hadi mwisho wa mwaka. Huduma za ulinzi wa amani za MONUC zinatarajiwa kuimarisha vizuri zaidi hali ya utulivu katika eneo hili la Afrika ya Kati.

Kadhalika ripoti ya MONUC juu ya uteklelezaji wa haki za binadamu katika DRC kwa Aprili imesema UM haukiridhika na mchango wa vuguvugu kutoka kwa wenye madaraka wakati MONUC ilipoendeleza uchunguzi kuhusu fujo zilizotukia Kinshasa mwisho wa mwezi Machi, baada ya uchaguzi kufanyika. Ripoti ilitilia mkazo kwamba licha ya MONUC kupatiwa msaada dhaifu na wenye madaraka, wataalamu wanaohusika na masuala ya haki za binadamu walifanikiwa kukusanya ushahidi yakini kuhusu matukio hayo, baada ya kuwahoji watu 200 ambao walithibitisha kwamba maofisa wa usalama nchini DRC waliwatishia adhabu wale waathiriwa wa mapigano na watumishi wa afya waliotoa ushahidi wa tukio la baada ya uchaguzi, kwa wachunguzi wa UM.