Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazao ya nafaka 2007 kuvunja rikodi: FAO

Mazao ya nafaka 2007 kuvunja rikodi: FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) linaashiria uzalishaji wa mazao ya nafaka duniani kwa 2007 utavunja rikodi na kuongezeka kwa asilimia 5. Jumla ya mazo ya nafaka inabashiriwa kufikia tani milioni 2,095.

Kadhalika FAO inaashiria nchi 33, wingi wao zikiwa katika bara la Afrika - ikijumuisha Kenya, Uganda na Tanzania - zitahitajia kuhudumiwa misaada ya dharura ya chakula kwa sababu ya kujiri kwenye maeneo yao hali ya hewa mbaya. Mataifa mengine katika Afrika ambayo vile vile yatahitajia msaada wa chakula ni yale ya Ethiopia, Eritrea, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Usomali, maeneo yalioathiriwa na vurugu, hali ya mapigano na ukame ulionea kwa muda mrefu na kutowapatia raia fursa ya kupandisha na kuvuna nafaka maridhawa ili kukidhia mahitaji ya chakula ya umma.