Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Ulinzi wa Haki za Binadamu Duniani, Louise Arbour ameshtumu vikali muongezeko wa vurugu na mapigano yaliofumka karibuni kwenye Tarafa ya Ghaza, na ametoa mwito maalumu wenye kuhadharisha pande zote husika na mgogoro huu kutokiuka kanuni za kiutu za kimataifa, sheria ambazo zinawajibisha wenye madaraka kuhakikisha raia wote wanaojikuta wamenaswa kwenye mapigano kupatiwa hifadhi.~

•Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) limetunukia, kwa mara ya kwanza, Tunzo ya ILO juu ya Hishima ya Kazi, kwa Raisi Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela pamoja na Carmelo-Mesa Lago, Profesa wa Uchumi na Mafunzo ya Amerika ya Latina katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh kwenye Jimbo la Pennsylvania, Marekani.

•Baraza Kuu la UM limemteua Srgjan Kerim wa iliokuwa Jamhuri ya Yugoslavia ya Macedonia kuwa Raisi wa kikao kijacho cha 62 cha Baraza Kuu ambacho kinatazamiwa kuanza shughuli zake mwezi Septemba 2007.