Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya mfumo wa vikosi vya amani kwa Darfur imekamilishwa

Ripoti ya mfumo wa vikosi vya amani kwa Darfur imekamilishwa

KM Ban Ki-moon amemtumia Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Mei, Balozi Zalmay Khalilzad wa Marekani na vile vile Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika (AU), ripoti yenye kuelezea, kwa ukamilifu, mfumo wa vikosi vya mseto vya AU na UM vinavyotazamiwa kupelekwa kwenye jimbo la Sudan magharibi la Darfur.

Kadhalika, Mwenyekiti wa Tume Kuu ya AU, Alpha Oumar Konare, baada ya kushauriana na KM wa UM Ban Ki-moon wameafikiana kumteua Jenerali Martin L. Agwai wa Nigeria kuwa Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Amani vya AU Sudan (AMIS), kwa matarajio kuwa katika siku zijazo atachukua madaraka ya kuongoza, vile vile, Vikosi vya Mseto vya AU/UM kwa Darfur.