Skip to main content

Halali kutuma vikosi vya usalama CAR, asisitiza Mshauri wa UM juu ya misaada ya dharura

Halali kutuma vikosi vya usalama CAR, asisitiza Mshauri wa UM juu ya misaada ya dharura

Mshauri wa KM kwa Masuala ya Kiutu, John Holmes alipendekeza, kwenye ripoti aliowasilisha mbele ya Baraza la Usalama (BU) kuhusu ziara ya karibuni barani Afrika, kuwa wakati umewadia kwa jamii ya kimataifa kupeleka vikosi vya amani vya kimataifa, vyenye ujuzi na uzoefu mbalimbali, kwenye lile eneo la vurugu la Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), liliopo kaskazini mashariki ambapo karibuni wakazi 300,000 walingo\'lewa makwao kwa nguvu kwa sababu ya mapigano yaliofumka huko na kuhatarisha maisha ya raia.Holmes alipendekeza vikosi vya kimataifa vipelekwe bila ya kusubiri idhini ya taifa jirani la Chad, ambalo kwa sasa nalo pia limezongwa na mvutano wa uhasama wa wenyewe kwa wenyewe.