Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

WHO imepongeza uamuzi wa karibuni wa kampuni ya madawa ya Maabara ya Abbott (Abbott Laboratories) wenye dhamira ya kupunguza bei ya zile dawa za kurefusha maisha zinazojulikana kama LPV/R, ambazo huuzwa kwenye soko la kimataifa kwa kutumia jina la Kaletra/Aluvia, na hupewa wagonjwa wenye VVU na UKIMWI.~

Josette Sheeran, wa Marekani, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) ameanza kazi rasmi majuzi, na alitoa mwito maalumu wa kuihimiza jamii ya kimataifa kuendelea kuzitekeleza zile ahadi za kuwapatia chakula maridhawa, na kwa wakati, umma bilioni moja muhitaji uliopo sehemu mbalimbali duniani, hasa ilivyokuwa idadi ya watu wanaosumbuliwa na utapia mlo inaongezeka duniani kwa milioni 4 kila mwaka.

KM Ban Ki-moon aliwaambia wawaklilishi wa kimataifa waliohudhuria kikao cha Kamisheni ya Kupunguza Silaha, kilichofanyika Makao Makuu mjini New York, kwamba hajaridhika na maendeleo haba yaliojiri kwenye zile juhudi za kimataifa katika kukabiliana na hatari ya silaha za mauaji ya halaiki.

[na mwishowe] Salvano Briceno, Mkurugenzi wa Taasisi ya UM juu ya Miradi ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa (UN/ISDR) iliopo mjini Geneva, ametoa onyo linalosema ulimwengu unahitajia juhudi za dharura kudhibiti vilivyo athari haribifu zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, mabaki ambayo hudhuru afya za umma na maisha, kwa ujumla.