Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za UM kudhibiti maradhi ya vijidudu vinavyodhuru ngano

Juhudi za UM kudhibiti maradhi ya vijidudu vinavyodhuru ngano

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti kugundua aina ya vijidudu vijiyoga vipya, vyenye uwezo wa kuzusha maambukizo haribifu makubwa ya mazao ya ngano, vijidudu ambavyo vimeshuhudiwa kusambaa kwenye maeneo yalioanzia Afrika Mashariki - ikijumuisha mataifa ya Ethiopia, Kenya na Uganda – na kuenea hadi Yemen, kwenye Ghuba ya Bara Arabu.

Shirika la FAO, limekadiria asilimia 80 ya aina zote za mbegu za ngano zinazopandishwa katika Afrika na Asia, hukabiliwa na hatari ya maambukizo ya vijiyoga kutu haribifu. Inahofiwa vijidudu hivi kama havijadhibitiwa mapema, huenda vikaenea kuenea kwa kasi kwenye maeneo husika, hasa katika zile sehemu ambazo hupandisha mazao ya ngano kwa wingi, na baadaye kuleta hasara inayokisiwa kuzidi mabilioni kadha ya dola za Kimarekani.

Sikiliza ripoti zaidi kwenye iidhaa ya mtandao.