Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kimataifa kupiga vita shurua zaonesha mafanikio

Juhudi za kimataifa kupiga vita shurua zaonesha mafanikio

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zilithibitisha, kwa muda mrefu sasa, ya kwamba ugonjwa wa shurua bado unaendelea kusumbua mamilioni ya watoto na kusababisha vifo, hususan miongoni mwa watoto chini ya umri wa miaka mitano walikosa kupatiwa chanjo kinga dhidi ya shurua.~

Katika 2001, UM na mashirika kadha wenzi, yalijumuika na kuanzisha mpango mpya ya kupambana na shurua, mradi ambao ulilenga kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaoambukizwa nayo, kwa asilimia 90, itakapotimia 2010.

Mnamo miaka mitano ya kwanza ya kampeni hiyo watoto wachanga milioni 360 ziada duniani walifanikiwa kupatiwa chanjo kinga dhidi ya shurua, hususan katika bara la Afrika.

Kwa maelezo kamili sikiliza idhaa ya mtandao.