Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha miaka 200 ya kupiga marufuku biashara ya utumwa

UM waadhimisha miaka 200 ya kupiga marufuku biashara ya utumwa

Umoja wa Mataifa ulishiriki, hivi majuzi, kwenye taadhima mbalimbali za kumbukumbu ile siku biashara ya utumwa ilipigwa marufuku na Bunge la Uingereza.

Katika mwezi Novemba 2006, Baraza Kuu la UM lilipitisha azimio malumu liliopendekeza tarehe 25 Machi 2007 iadhimishwe kuwa ni Siku ya Kumbukumbu za Kimataifa juu ya Kukomeshwa Biashara ya Utumwa kwenye Maeneo ya Ng’ambo ya Atlantiki, azimio ambalo lilikumbusha kwamba biashara ya utumwa ndio “kiini hakika kilichochea kuwepo pengo kubwa la ukosefu wa hali ya usawa, wa kiuchumi na jamii, kwenye karne ya sasa, dhidi ya watu wenye asili ya Kiafrika, urithi ambao, vile vile azimio lilisitiza, umeeneza chuki, madhara ya kutovumiliana na ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Kiafrika, waliotawanyika, pote duniani."

Tumejumuisha kwenye kipindi ripoti juu ya kumbukumbu hizo za UM za kukomesha utumwa, pamoja na kukupatieni mahojiano mafupi, na Profesa Ali Mazrui wa Chuo Kikuu cha Jimbo la New York (Binghamton) ambaye anazungumzia hasara na athari za utumwa kwa vizazi vya sasa vya watu wenye asili ya Kiafrika katika mataifa yalioshiriki kwenye biashara ya utumwa katika karne ziliopita.