Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Ripoti iliotolewa shirika na Jumuiya ya UNAIDS, UNICEF na WHO imearifu ya kuwa takriban mataifa yote ulimwenguni yameonesha mafanikio fulani fulani kwenye matibabu ya UKIMWI, lakini hata hivyo, bado kutahitajika mchango mkubwa wa kimataifa kwa walimwengu kuweza kuzipatia nchi zote muhitaji matibabu yanayofaa katika 2010, kama ilivyodhamiriwa na Mataifa Wanachama.

Mshauri wa KM juu ya Watoto Walionaswa kwenye Hali ya Mapigano, Radhika Coomaraswamy ambaye hivi karibuni alikamilisha ziara ya uchunguzi katika Lebanon, Israel na maeneo yaliokaliwa kimabavu ya Falastina, alinakiliwa akisema ukaguzi wake umethibitisha watoto wadogo ndio wenye kuumizwa na kudhurika zaidi na athari za hali ya mapigano katika Mashariki ya Kati.

Ripoti ya karibuni ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imethibitisha kihakika ya kuwa chanzo cha vifo kwa vijana kati ya umri wa miaka 10 hadi 24 duniani hutokana na ajali za magari barabarani, ambazo huua vijana 400,000 na kujeruhi mamilioni ziada; WHO imependekeza vijana wote wa kimataifa wapatiwe mafunzo kinga kuhusu kanuni za usalama barabarani.