Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serekali ya Uganda yanasihiwa kurekibisha sera ya kusalimisha silaha katika Karamoja

Serekali ya Uganda yanasihiwa kurekibisha sera ya kusalimisha silaha katika Karamoja

Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Ulinzi wa Haki za Binadamu ametoa ripoti wiki hii iliorudia tena pendekezo la kuitaka Serekali ya Uganda kufanya mapitio ya kurekibisha sera ya kuwalazimisha watu kusalimisha silaha kwenye eneo la Karamoja, kaskazini mashariki ya Uganda.