Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon aliwanasihi wajumbe wa kimataifa waliohudhuria Kikao cha Saba juu ua Demokrasia, Maendeleo na Biashara Huru, kilichofanyika Doha, Qatar kuhakikisha duru yao ya mazungumzo itawasilisha mafanikio ya kuridhisha, maana bila ya kuyafannya hayo, alionya, nchi masikini zitaporomoka zaidi kimaendeleo, hali ambayo anaamini itafumsha mitafaruku na kueneza hali ya wasiwasi kwenye mfumo mzima wa biashara katika soko la kimataifa.~

•Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Vijana Duniani ulioandaliwa na UM mjini Geneva, na kuhudhuriwa na vijana 400 kutoka kanda mbalimbali za dunia, umepitisha azimio la kuhamasisha serekali, maskuli, vyuo vikuu, vyombo vya mawasiliano ya habari, na pia mashirika yanayohusika na viwanda vya burudani pamoja na vijana wenyewe, kuchukua hatua za haraka, kitaifa na kimataifa, ili kuboresha usalama wa barabarani kwa vijana.

• KM Ban Ki-moon amemteua Raisi Mstaafu wa Ureno, Jorge Sampaio kuwa Mwakilishi Mkuu mpya juu ya Masuala ya Ushirikiano wa Tamaduni, uteuzi ambao ulifanyika baada ya KM Ban kushauriana na Wakuu wa Serekali za Uspeni na Uturuki, wadhamini bia wa Muungano wa Kuimarisha Ushirikiano wa Tamaduni Tofauti Kimataifa.