Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imeanzisha operesheni za kuhudumia waathiriwa wa kimbunga Bukini

WFP imeanzisha operesheni za kuhudumia waathiriwa wa kimbunga Bukini

Shirika la WFP limeanzisha misafara ya ndege, za kupeleka chakula na misaada ya dharura inayohitajika kuwahudumia kihali maelfu ya watu wanaoishi kaskazini-magharibi ya Bukini, eneo ambalo hivi karibuni lilichafuliwa vibaya na kimbunga kilichoharibu vibaya sana barabara na madaraja.

Huduma za WFP Bukini zinatazamiwa kuchukua wiki nne, na zitatumia helikopta kupeleka chakula na misaada mengineyo ya kiutu kwa wanavijiji 20,000 waliodhurika zaidi na janga la kimbunga.