Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inaripoti kuwepo vitendo vya chuki dhidi ya wahamiaji wa Usomali Afrika Kusini

UNHCR inaripoti kuwepo vitendo vya chuki dhidi ya wahamiaji wa Usomali Afrika Kusini

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kutukia vitendo vya ubaguzi dhidi ya wahamiaji wa Kisomali waliopo Afrika Kusini.

UNHCR ilisema kwamba kwa mujibu wa madai ya Jumuiya ya Wasomali katika Afrika Kusini wenziwao 400 waliuawa katika miaka kumi iliopita kwa sababu ya vitendo vya chuki dhidi ya wageni.

Serekali ya Afrika Kusini imeahidi kuchunguza maafa haya na kuchukau hatua za haraka kuhakikisha wahamiaji wanapatiwa hifadhi na ulinzi. Nosiviwe Mapisa-Nqakula, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini ameripotiwa akisema kwamba ile Sheria ya Wahamiaji ya 1996 inatazamiwa kubadilishwa na kurekibishwa katika mwaka huu, kwa madhumuni ya kuboresha uongozaji wa huduma za wahamiaji nchini.