Mapendekezo ya KM kurekebisha shughuli za UM yaungwa mkono na Baraza Kuu

16 Machi 2007

Baraza Kuu la UM Alkhamisi limepitisha maazimio mawili muhimu ya kuunga mkono mapendekezo ya KM Ban Ki-moon ya kuleta mageuzi katika kazi za taasisi hii muhimu ya kimataifa. Azimio la kwanza linalenga Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani (DPKO), na limekusudiwa kuboresha kazi za Idara kwa kuipatia uwezo wa kupeleka haraka vikosi vya UM kulinda amani kwenye maeneo yenye machafuko. Vile vile azimio limetaka kubuniwe Kitengo cha Idara juu ya Huduma za Amani Nje ya Makao Makuu.

Baada ya maazimio haya mawili kupitishwa KM Ban aliwashukuru wawakilishi wa kimataifa kwenye Baraza Kuu kwa kumthibitishia imani yao juu ya uongozi wake kwa kupitisha maazimio aliyoyapendekeza, ya kuleta mageuzi na kuboresha kazi na shughuli za UM kijumla. Alipongeza kwamba ushirikiano kati ya Mataifa Wanachama na KM unaanza kwa mguu mzuri, na ni matumaini yake utaendelezwa kwa sauti moja - uhusiano ambao, alitilia mkazo, umejengeka kwa msingi wa kuaminiana.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter