Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki halali za wenyeji wa asili, na athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Haki halali za wenyeji wa asili, na athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Baraza jipya la UM juu ya Haki za Binadamu lilipitisha, mnamo tarehe 29 Juni 2006, Azimio la Mwitiko wa Kuimarisha Haki za Wenyeji wa Asli Duniani. Azimio hili lilifanikiwa kupitishwa baada ya kufanyika kampeni ya miaka ishirini ziada, ambapo jumuiya zinazowakilisha jamii za wenyeji wa asili zilishirikiana na taasisi za Umoja wa Mataifa kadha wa kadha, na hatimaye, kuweza kuratibu mswada wa kuridhisha uliokuwa na makusudio ya kuwapatia wenyeji wa asili ulinzi wa kisheria na hifadhi bora ya haki za kimsingi, na za kijadi, halkadhalika. ~~

Sikiliza kwenye idhaa ya mtandao taarifa kamili kuhusu suala hili; na vile vile sikiliza mahojiano na mwenyeji wa asili kutoka Kajiado, Kenya akizungumzia athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye ardhi zao za kijadi.