Hapa na pale

23 Machi 2007

Baraza la Haki za Binadamu limefanyisha mjadala maalumu wiki hii mjini Geneva kuzingatia suala la kukomesha vitendo vya kutumia nguvu dhidi ya watoto, janga karaha ambalo linakiuka maadili ya kiutu.~

Na hatimaye KM Ban Ki-moon amesema anaunga mkono kuanzishwa kwa serekali ya muungano ya Falastina, kitendo ambacho alipiongeza kuwa ni hatua muhimu katika kusukuma mbele ujenzi wa amani Mashariki ya Kati; lakini vile vile alidhihirisha masikitko Serekali ya Muungano ya Falastina bado haikufanikiwa kuyatekeleza matakwa ya kundi la wapatanishi wanne kuhusu suluhu ya Mashariki ya Kati.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter