Eritrea imemfukuza nchi mtaalamu wa UM juu ya mabomu ya kutegwa

23 Machi 2007

Serekali ya Eritrea imeiarifu UM kumpiga marufuku nchini, Meneja wa Mradi wa UM unaosimamia Ufyekaji wa Mabomu Yaliotegwa Ardhini, David Bax kwa madai kuwa alikiuka sheria na kanuni za nchi. Shirika la UM linalosimamia uangalizi wa Eneo la Amani Mipakani kati ya Ethiopia na Eritrea (UNMEE) limeripoti kutokubaliana na madai hayo ya Serekali ya Eritrea. Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti za UNMEE, Bax ameshaondoka Eritrea kwa hivi sasa.~

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter