Skip to main content

Makumi elfu ya raia wameuhama mji baada ya kutukia mapigano katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR)

Makumi elfu ya raia wameuhama mji baada ya kutukia mapigano katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR)

UM imeripoti ya kuwa raia 14,000 wameyahama makazi katoka mji wa kaskazini-mashariki katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kufumka mapigano mwanzo wa mwezi kati ya majeshi ya Serekali na makundi ya waasi.

Kwa mujibu wa Toby Lanzer, mshauri wa UM kuhusu misaada ya kiutu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, asilimia 70 ya nyumba za wakazi wa eneo hilo la mapigano zilichomwa moto kwa makusudi makundi yanayopigana na kusababisha uharibifu uliokiuka mipaka.