Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasaidia Wakongomani 35 kuhajiri Marekani kuanza maisha mapya

UNHCR yasaidia Wakongomani 35 kuhajiri Marekani kuanza maisha mapya

Kundi la kwanza la Wakongomani 35, kati ya 500 walionusurika mauaji ya halaiki katika Burundi, wanatarajiwa karibuni kuanza safari ya uhamishoni Marekani kuanzisha maisha mapya. Msaada huu ulichangiwa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamaiji (UNHCR).

Makazi mapya ya Wakongomani hawa yanatarajiwa kuwa katika miji ya Marekani ya Denver, Louisville na San Fransisco.