Mripuko wa uhasama na mapigano Kinshasa walaaniwa na UM

23 Machi 2007

KM wa UM Ban Ki-moon, pamoja na wawakilishi wa Baraza la Usalama na pia Shirka linalosimamia huduma za ulinzi wa amani katika JKK (MONUC), wote kwa kauli moja wameshtumu mapigano yaliozuka karibuni katika mji mkuu wa DR Congo wa Kinshasa, kati ya vikosi vya Serekali na walinzi wa aliyekuwa Naibu-Raisi Jean-Pierre Bemba.

KM ametoa mwito unaopendekeza mapigano yasitishwe, halan, na makundi yote husika na mgogoro ambao alionya unahatarisha maisha ya raia na huenda ukakoroga utulivu wa amani uliopo nchini kwa sasa. MONUC imeripoti kuwa tayari kuisaidia Serekali ya DR Congo kudhibiti hali ya mapigano na, hatimaye, kurudisha usalama wa eneo; na wakati huo huo MONUC itajuhusisha katika juhudi za kutafuta suluhu ya kuridhisha kuhusu ulinzi na usalama wa Bemba.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter