Ziara ya faragha ya KM katika Iraq

23 Machi 2007

KM Ban Ki-moon Alkhamisi alifanya ziara ya fargha ya siku moja katika Iraq. Wakati alipokuwa huko alikutana kwa mazungumzo, mjini Baghdad na Waziri Mkuu Nouri Kamal al-Maliki na kuzungumzia juu ya mchango wa UM katika kuusaidia umma wa Iraq kurudisha utulivu wa amani na maendeleo kwenye taifa lao.

Baraza la Usalama lilitoa taaarifa rasmi ya kuunga mkono safari ya KM Ban Ki-moon katika Iraq. Taarifa ilisema inakubalina, kwa kauli moja, na juhudi za KM za kuleta amani na upatanishi wa makundi yanayohasimiana katika Iraq. Kadhalika, taarifa ya Baraza la Usalama ilishtumu vikali shambulio liliotukia, na kutafsiriwa kuwa ni la kigaidi, dhidi ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq wakati Waziri Mkuu na KM Ban walipokuwa wakikutana na waandishi habari.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter