Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya kimataifa kunuia vita dhidi ya TB

Jamii ya kimataifa kunuia vita dhidi ya TB

Alkhamisi, Jorge Sampaio, Mjumbe Maalumu wa KM katika Kukomesha Maradhi ya Kifua Kikuu/TB aliwakilisha mbele ya waandishi habari wa kimataifa, hapa Makao Makuu, ripoti maalumu iliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu udhibiti bora wa maradhi ya kifua kikuu.TB duniani.

Alisema kuenea kwa uhusiano wa virusi vya UKIMWI maututi na TB ni tatizo liliofichukana kuongezeka kwa kasi duniani, na linakithirisha vifo vya wagonjwa wa UKIMWI, hasa katika mataifa ya Afrika kusini ya Sahara, ambapo ndipo janga la TB liliposelelea zaidi.

Ripoti hii mpya ya WHO kuhusu udhibiti wa TB ulimwenguni imethibitisha ya kuwa kiwango cha maambukizo ya ugonjwa huu hakitarajiwi, kwa hivi sasa, kupanda wala kushuka tena. Lakini mafanikio haya hayyawezi kuendelezwa na yamezorotishwa na tatizo la kuenea kwa virusi vya UKIMWI duniani, pamoja na kuwepo dawa sugu zenye tiba kapa, na uhaba wa misaada ya kuridhisha ya kimataifa inayohitajika kukabiliana na tatizo hili la afya kama inavyotakiwa. Mradi wa Kufyeka TB Kimataifa, unao’ongozwa na Shirika la WHO, unahitajia msaada wa dola bilioni 56 kufidia huduma za kudhibiti TB kati ya miaka ya 2006 hadi 2015.